Habari, Taarifa, Matamko na Matukio

Mwenyekiti wa BAVICHA KIGAMBONI, ndugu Sheila Mchamba akimnadi mgombea wa uenyekiti wa serikali ya mtaa kwenye mtaa anakoishi yeye maweni. Ndg Sheila amejadili zaidi kwenye umuhimu wa kuwapa vijana nafasi za kuongoza mitaa yao kwasababu wameonesha uthubutu kwenye kutatua changamoto zinaziwakabili wanajamii wenzao

Mwenyekiti wa Bawacha wilaya ya Kigamboni (ambae pia ni mgombea ujumbe wa serikali ya mtaa, mtaa wa maweni) akinadi sera zake kwa wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika tarehe 27/11/2024

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee BAZECHA, Ndugu Othman Makono akinadi sera na wagombea kwenye mkutano wa kampeni kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa, vijiji na vitongoji utakofanyika tar 27/11/2024

Katibu wa Chama wilaya ya Kigamboni Ndg Mussa Bwashari, azindua rasmi ilani ya uchaguzi kwenye mtaa anaogombea yeye, mtaa wa mbwamaji. Ilani hii imegusa maeneo muhimu ambayo anatarajia kwenda kuyafanyia kazi akipata ridhaa ya wananchi kuwa mwenyekiti wa mtaa huu

Katibu wa BAVICHA wilaya ya kigamboni, ndg Ezekiel Molel akizungumza na wanachama na viongozi wa mbwamaji kwenye uzinduzi wa ilani ya uchaguzi kwenye mtaa huo

Katibu wa Chama wilaya ya Kigamboni ndg Mussa Bwashari, akiwa kwenye zoezi la kurudisha fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa katika mtaa wa mbwamaji

Chadema kigamboni

You have been successfully Subscribed! Ops! Something went wrong, please try again.

MAWASILIANO

Info@kandayapwani.com

+123456789

1720, Kigamboni, Dar es salaam, Tanzania

© 2024 Chadema Tanzania

Scroll to Top