Habari, Taarifa, Matamko na Matukio
Mwenyekiti wa BAVICHA KIGAMBONI, ndugu Sheila Mchamba akimnadi mgombea wa uenyekiti wa serikali ya mtaa kwenye mtaa anakoishi yeye maweni. Ndg Sheila amejadili zaidi kwenye umuhimu wa kuwapa vijana nafasi za kuongoza mitaa yao kwasababu wameonesha uthubutu kwenye kutatua changamoto zinaziwakabili wanajamii wenzao
Mwenyekiti wa Bawacha wilaya ya Kigamboni (ambae pia ni mgombea ujumbe wa serikali ya mtaa, mtaa wa maweni) akinadi sera zake kwa wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika tarehe 27/11/2024
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee BAZECHA, Ndugu Othman Makono akinadi sera na wagombea kwenye mkutano wa kampeni kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa, vijiji na vitongoji utakofanyika tar 27/11/2024
Katibu wa Chama wilaya ya Kigamboni Ndg Mussa Bwashari, azindua rasmi ilani ya uchaguzi kwenye mtaa anaogombea yeye, mtaa wa mbwamaji. Ilani hii imegusa maeneo muhimu ambayo anatarajia kwenda kuyafanyia kazi akipata ridhaa ya wananchi kuwa mwenyekiti wa mtaa huu
Katibu wa BAVICHA wilaya ya kigamboni, ndg Ezekiel Molel akizungumza na wanachama na viongozi wa mbwamaji kwenye uzinduzi wa ilani ya uchaguzi kwenye mtaa huo
Katibu wa Chama wilaya ya Kigamboni ndg Mussa Bwashari, akiwa kwenye zoezi la kurudisha fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa katika mtaa wa mbwamaji