“Katibu Mkuu anawatangazia wanachama wote kuwa kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Chama na Mabaraza kwa ngazi ya Taifa utakaofanyika Januari, 2025. Fomu za kuomba kugombea nafasi za uongozi ngazi ya Taifa zinapatikana ofisi za Makao Makuu ya Chama, Makao Makuu ya Mabaraza, Ofisi za Kanda, Ofisi za Chama za Mikoa na Wilaya kuanzia tarehe 17/12/2024.” Mhe. @jjmnyika
“Ratiba ya Mikutano Mikuu ya Chama na Mabaraza itakuwa kama ifuatavyo; 1. Mkutano Mkuu wa Bavicha – 13 Januari, 2025 2. Mkutano Mkuu wa Bazecha – 13 Januari, 2025 3. Mkutano Mkuu wa Bawacha – 16 Januari, 2025 4. Mkutano Mkuu wa Chama – 21 Januari, 2025″ Mhe. @jjmnyika
Katika kipindi hiki cha uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea, Katibu Mkuu wa Chama, ninawataka wanachama na viongozi kuzingatia Katiba, Kanuni, Maadili ya Wanachama na Viongozi pamoja na Miongozo mbalimbali ya Chama…”
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEA CHADEMA WILAYA YA KIGAMBONI, katika zoezi la uchaguzi wa serikali ya mitaa, vijiji na vitongoji, kimefanikiwa kusimamishabwagombea 44 katika jumla ya mitaa 67 kwenye wilaya hiyo. Aidha kwenye zoezi la kuenguliwa wagombea wameunguliwa wagombea wawili, hivyo kusalia wagombea 42.